Monday, 31 March 2014

MAREKANI HAINA UHALALI WA KUIKOSOA URUSI

Ni takribani zaidi ya mwezi mmoja sasa dunia imekuwa kwenye mvutano mkubwa kufuatia mzozo wa mataifa makubwa kati ya Marekani na washirika wake dhidi ya Urusi kufuatia hatua ya Urusi kuingia kijeshi mashariki mwa Ukraine katika Jimbo la Crimea kwa kile ilichodai ni kulinda maslahi yake yaliyopo ndani ya nchi hiyo.

Raisi Barrak Obama

Hatua hiyo ya Urusi ilpingwa vikali na Marekani pamoja na washirika wake Uingereza,Ujerumani na Ufaransa kwa madai yakua hatua hiyo ni kuingilia mambo ya ndani ya taifa hilo la Ukraine na ni kinyume cha sheria za kimataifa pamoja na haki za binadamu.

Hatua ya Marekani na washirika kulaumu Urusi kwa hatua yake hii imenishangaza na kunisikitisa sana na haikuwa na uhalali wakuitoa kwani wao ndio wavunjifu wakubwa wa sheria za kimataifa na pamoja na haki za binadamu kwani imeshuhudiwa kila kukicha ikiuwa watu katika nchi mbalimbali kama vile Afghanistan,Pakistan,Iraq na hata Syria.

Inashangaza kuona Marekani ikikosoa Urusi huku majesshi yake yakiendelea kuua wanawake na watoto wasio na hatia.Marekani iliivamia Iraq mwaka 2003 bila ya idhini ya Umoja wa mataifa kwa madai ya kuwa inamiliki siliha za nyukilia na kufanikiwa kumuondoa madarakani Raisi wa zamani wa nchi hiyo Saadam Husein.Licha ya kufanikiwa kuingia Iraq bado hadi leo imeshindwa kuthibisha madai hayo.

Pia ili shirikiana na waasi wa Libya kumuondoa madarakani kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gadaf na sasa imepeleka baadhi ya maofisa wake wa kijeshi kutoa mafunzo ya kivita kwa waasi wa Syria wanaopigana kutaka kumuondoa madarakani Raisi Bashir Al-assad.Inafahamika waazi yote Marekani inayafanya haya kwa lengo la kupata maslahai hususa ya mafuta na gesi yaliyopo katika nchi hizo.

Inafahamika wazi kuwa Urusi in masrahi makubwa katika nchi ya Ukraine kutokana na nchi hiyo kuwa na inanunua mafuta na gesi kutoka kwake pia ina ushirikiano mkubwa wa kibiashara yeye vilevile zaidi ya asilimia 90 ya mabomba ya kuuzia mafuta na gesi ya Urusi kwenda Ulaya ya Magharibi yanapitia katika nchi hii ya Ukraine lakini maslahi haya yote yalikuwepo wakati wa utawala wa zamani Victor Youxshenko.

Kwa hiyo hali yoyote ile kuondolewa kwake madarakani kutabadilisha hali ya mambo na ndio maana Urusi imeamua kuingia kijeshi ili kuyalinda kinguvu na hatua siajabu kwa mataifa yenye nguvu kuyavamia kijeshi mataifa madogo.Hivyo kitendo cha Marekani na washirika wake kuilaumu Urusi kwa hatua hiyo haina uhalali kwani nao wanafanya hivohivo katika nchi nyingine hususani za Mashariki ya kati na Afrika Kaskazini.



























in

Thursday, 27 March 2014

WAKAZI WA MABONDENI ANZENI KUCHUKUA HATUA

Jana na leo kumeanza kushuhudiwa mvua kubwa katika jiji la Dar es salaam na maeneo mengine hapa nchini ambapo kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa hapa nchini wamezitaja kuwa ni mwanzo wa mvua za masika na zitaendelea kunyesha mpaka mwezi ujao.

Akizungumza na Shirka la utangazaji Tanzania (TBC), Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Dk.Agnes Kijazi amesema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini ni mvua za masika na zitaendelea kunyesha kwa wingi katiaka kipindi chote cha mwezi huu na mwezi ujao.

Kufuatia taarifa hiyo kutoka kwa Mamlaka ya hali ya hewa inayoeleza kuwepo kwa mvua nyingi hapa nchini katika kipindi hiki naomba nichukue nafasi hii kuwaomba ndugu zangu wale wanaoishi maeneo ya mabondeni kuweza kuhama kabla ya madhara kutokea.

Kila mwaka kumekuwa na madhara makubwa ambayo yanatokea kwa wakazi waishio mabondeni pindi zinyeshapo mvua.Hivyo ni vyema watu wakaanza kuchuka tahadhari mapema ili kuepusha madhara na gharama kubwa ya kuhudumiwa kutoka serikalini.

Licha ya madai yenu ya kusema hamna mahali pakwenda pindi mukiondoka katika maeneo yenu mulioyazoea na hata maeneo muliyopangiwa na serikali kama vile mabwepande kuwa ni mbali na mno na maeneo ya kati ya mji amboyo ndio hutumika kufanyia shughuli mbalimbali za maisha kimsingi bado nataka kusisitiza kuwa bado madhara ya mafuriko ni makubwa kwani yanaweza kugharimu maisha ya watu hususani kina mama na watoto ambao ndio huwa wahanga wakubwa wajanga pindi yatokeapo.