Thursday, 27 March 2014

WAKAZI WA MABONDENI ANZENI KUCHUKUA HATUA

Jana na leo kumeanza kushuhudiwa mvua kubwa katika jiji la Dar es salaam na maeneo mengine hapa nchini ambapo kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa hapa nchini wamezitaja kuwa ni mwanzo wa mvua za masika na zitaendelea kunyesha mpaka mwezi ujao.

Akizungumza na Shirka la utangazaji Tanzania (TBC), Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Dk.Agnes Kijazi amesema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini ni mvua za masika na zitaendelea kunyesha kwa wingi katiaka kipindi chote cha mwezi huu na mwezi ujao.

Kufuatia taarifa hiyo kutoka kwa Mamlaka ya hali ya hewa inayoeleza kuwepo kwa mvua nyingi hapa nchini katika kipindi hiki naomba nichukue nafasi hii kuwaomba ndugu zangu wale wanaoishi maeneo ya mabondeni kuweza kuhama kabla ya madhara kutokea.

Kila mwaka kumekuwa na madhara makubwa ambayo yanatokea kwa wakazi waishio mabondeni pindi zinyeshapo mvua.Hivyo ni vyema watu wakaanza kuchuka tahadhari mapema ili kuepusha madhara na gharama kubwa ya kuhudumiwa kutoka serikalini.

Licha ya madai yenu ya kusema hamna mahali pakwenda pindi mukiondoka katika maeneo yenu mulioyazoea na hata maeneo muliyopangiwa na serikali kama vile mabwepande kuwa ni mbali na mno na maeneo ya kati ya mji amboyo ndio hutumika kufanyia shughuli mbalimbali za maisha kimsingi bado nataka kusisitiza kuwa bado madhara ya mafuriko ni makubwa kwani yanaweza kugharimu maisha ya watu hususani kina mama na watoto ambao ndio huwa wahanga wakubwa wajanga pindi yatokeapo.

1 comment: