Monday, 14 April 2014

MZEE GURUMO HATASAHAULIKA NA WATANZANIA

Mzee Gurumo akiimba wakati wa uhai wake.
April 13, ni siku isiyosahaulika na watanzania wengi hususa wale wa tathnia ya muziki wa Dansi na hii ni baada ya kumpoteza nguli wa muziki huo nae simwingine bali ni marehemu Muhidini Gurumo ambaye alifariki asubuhi ya jana katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Gurumo alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu hali iliyomfanya astaafu shughuli za muziki mapema mwaka jana na anatarajiwa kuzikwa leo saa saba mchana kijijini kwao alikozaliwa mipango ya maziko inafanyika nyumbani kwa marehemu Tabata Makuburi jijini Dar es salaam.

Gurumo alizaliwa mwaka 1940 katika kijiji cha Msaki,Kisalawe Mkoani Pwani alianza kujishugulisha katika muziki wa Dansi mwanzoni mwa miaka ya sitini,ameimbia katika bendi mbalimbali hapa nchini zikiwemo DDC Mlimani Park,Bima na Msondo Ngoma Music Band.Pia mwanzilishi wa mtindo wa msondo.

Katika uhai wake marehemu alitoa mchango mkubwa katika tathnia hii kwa kutunga nyimbo mbalimbali kama vile Namshukuru Mjomba.Pia alikuwa akihariri nyimbo mbalimbali za Msondo zilizokuwa zikutungwa na wasanii mbalimbali wa bendi hiyo kama TX Moshi,Othmani Momba na wengi neo.


Tuesday, 1 April 2014

ZOEZI LA KUSAFISHA JIJI LINGEANZIA KATIKA HATUA YA KUZIBUA MITARO

Eneo la Kariakoo Jijini Dar es salaam
Kwa zaidi ya siku ya pili sasa katika Jiji la Dar es salaam kumeshuhudiwa operesheni ya kuwaondoa watu wanaofanya biashara katika maeneo yasio rasmi kama vile katika sehemu za kandokando ya barabara na  kwenye maeneo ya viwanja vya wazi kama vile katika viwanja za Zakhiem na mengineyo.

Licha ya operesheni hii kuwa na uhalali wa kisheria lakini imeonekana kuwa ni mwiba mchungu kwa wafanya biashara hao pamoja wateja wao na kusababisha malalamiko kutoka kila kona kutokana na kuona kama wao wanaonewa na Serikali yao.Hii inatokana na udhaifu mkubwa uliofanywa na Jiji wakuwaachia wao kufanya biashara  kwa muda mrefu bila ya kuchukulia hatua kyasi kuwafanya  wajione kama wapo kisheria katika maeneo hayo.

Wahusika waoperesheni hii wamedai kuwa zoezi hili linalenga kusafisha Jiji ili liwe katika mazingira ya usafi pamoja na kurudishwa maeneo ambayo yakitumika kama vile katika stendi za darara na viwanja vya wazi ili yatumike katika shughuli zake kama ilivyo kusudiwa.

Napenda kuwakumbusha watu wa halmashauri ya Jiji kuwa zoezi linaloendelea linaloitwa la kusafisha Jiji lilipaswa kuanzia katika hatua ya kuzibua mitaro ya maji iliyojazana uchafu hadi kushindwa kutiririsha maji kama ilivyo kusudiwa na kusababisha harufu mbaya kwa wakazi wa maeneo hayo na hata wapita njia.

Mitaro mingi iliyopo Dar es salaam hususa katika maeneo ya katikati ya Jiji haifanyi kazi kutokana na kujaa uchafu uliokithiri hatua ambayo inaweza kusababisha magonjwa ya mlipukuko kama vile kipindupindu hususa katika kipindi kama hiki cha majira ya mvua ambayo husababisha kujaa maji kwa mitaro hiyo na kufuluma hadi katika maeneo ya makazi ya watu.

Kwangu mimi binafsi suala la kuzibua mitaro ya maji ni la muhimu zaidi kuliko kuwa ondoa wafanya biashara kwani suala la afya ya binadamu ni la msingi zaidi kuliko kitu kingine. Vilevile kui
acha mitaro hiyo ikitoa harufu mbaya ni aibu kwa taifa ikizingatiwa Jiji la Dar es salaam ndio sehemu penye ofisi nyeti hapa nchini kama Ikulu na wizara mbalimbali.

Pia ndani ya Dar es saalam kuna ofisi mbalimbali za kimataifa kama ofisi za kidiplomasia hali inayo sababisha uingiaji mkubwa wa wageni kutoka nje ya nchi.Hivyo ni vyema halimashauri ya Jiji ingeanza na zoezi hili kwanza ili kuweka afya za Watanzania katika mazingira salama, pamoja na kuliweka Jiji katika taswira nzuri kwetu na hata kwa wageni waingiao hapa nchini