Monday, 14 April 2014

MZEE GURUMO HATASAHAULIKA NA WATANZANIA

Mzee Gurumo akiimba wakati wa uhai wake.
April 13, ni siku isiyosahaulika na watanzania wengi hususa wale wa tathnia ya muziki wa Dansi na hii ni baada ya kumpoteza nguli wa muziki huo nae simwingine bali ni marehemu Muhidini Gurumo ambaye alifariki asubuhi ya jana katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Gurumo alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu hali iliyomfanya astaafu shughuli za muziki mapema mwaka jana na anatarajiwa kuzikwa leo saa saba mchana kijijini kwao alikozaliwa mipango ya maziko inafanyika nyumbani kwa marehemu Tabata Makuburi jijini Dar es salaam.

Gurumo alizaliwa mwaka 1940 katika kijiji cha Msaki,Kisalawe Mkoani Pwani alianza kujishugulisha katika muziki wa Dansi mwanzoni mwa miaka ya sitini,ameimbia katika bendi mbalimbali hapa nchini zikiwemo DDC Mlimani Park,Bima na Msondo Ngoma Music Band.Pia mwanzilishi wa mtindo wa msondo.

Katika uhai wake marehemu alitoa mchango mkubwa katika tathnia hii kwa kutunga nyimbo mbalimbali kama vile Namshukuru Mjomba.Pia alikuwa akihariri nyimbo mbalimbali za Msondo zilizokuwa zikutungwa na wasanii mbalimbali wa bendi hiyo kama TX Moshi,Othmani Momba na wengi neo.


No comments:

Post a Comment