 |
Eneo la Kariakoo Jijini Dar es salaam |
Kwa zaidi ya siku ya pili sasa katika Jiji la Dar es salaam kumeshuhudiwa operesheni ya kuwaondoa watu wanaofanya biashara katika maeneo yasio rasmi kama vile katika sehemu za kandokando ya barabara na kwenye maeneo ya viwanja vya wazi kama vile katika viwanja za Zakhiem na mengineyo.
Licha ya operesheni hii kuwa na uhalali wa kisheria lakini imeonekana kuwa ni mwiba mchungu kwa wafanya biashara hao pamoja wateja wao na kusababisha malalamiko kutoka kila kona kutokana na kuona kama wao wanaonewa na Serikali yao.Hii inatokana na udhaifu mkubwa uliofanywa na Jiji wakuwaachia wao kufanya biashara kwa muda mrefu bila ya kuchukulia hatua kyasi kuwafanya wajione kama wapo kisheria katika maeneo hayo.
Wahusika waoperesheni hii wamedai kuwa zoezi hili linalenga kusafisha Jiji ili liwe katika mazingira ya usafi pamoja na kurudishwa maeneo ambayo yakitumika kama vile katika stendi za darara na viwanja vya wazi ili yatumike katika shughuli zake kama ilivyo kusudiwa.
Napenda kuwakumbusha watu wa halmashauri ya Jiji kuwa zoezi linaloendelea linaloitwa la kusafisha Jiji lilipaswa kuanzia katika hatua ya kuzibua mitaro ya maji iliyojazana uchafu hadi kushindwa kutiririsha maji kama ilivyo kusudiwa na kusababisha harufu mbaya kwa wakazi wa maeneo hayo na hata wapita njia.
Mitaro mingi iliyopo Dar es salaam hususa katika maeneo ya katikati ya Jiji haifanyi kazi kutokana na kujaa uchafu uliokithiri hatua ambayo inaweza kusababisha magonjwa ya mlipukuko kama vile kipindupindu hususa katika kipindi kama hiki cha majira ya mvua ambayo husababisha kujaa maji kwa mitaro hiyo na kufuluma hadi katika maeneo ya makazi ya watu.
Kwangu mimi binafsi suala la kuzibua mitaro ya maji ni la muhimu zaidi kuliko kuwa ondoa wafanya biashara kwani suala la afya ya binadamu ni la msingi zaidi kuliko kitu kingine. Vilevile kui
acha mitaro hiyo ikitoa harufu mbaya ni aibu kwa taifa ikizingatiwa Jiji la Dar es salaam ndio sehemu penye ofisi nyeti hapa nchini kama Ikulu na wizara mbalimbali.
Pia ndani ya Dar es saalam kuna ofisi mbalimbali za kimataifa kama ofisi za kidiplomasia hali inayo sababisha uingiaji mkubwa wa wageni kutoka nje ya nchi.Hivyo ni vyema halimashauri ya Jiji ingeanza na zoezi hili kwanza ili kuweka afya za Watanzania katika mazingira salama, pamoja na kuliweka Jiji katika taswira nzuri kwetu na hata kwa wageni waingiao hapa nchini